Tell your friends about this item:
Tambua Na Tumikia Kusudi La Mungu Maishani Mwako Dr Gerson Mgaya
Tambua Na Tumikia Kusudi La Mungu Maishani Mwako
Dr Gerson Mgaya
Kila mtu amekuja duniani kwa kusudi maalum. Hakuna mtu anayekuja kwa bahati mbaya! Lakini ukisoma Mwanzo 6 utaona habari za viumbe waliofahamika kama wanefili. Hawa hawakuwa binadamu kwa asilimia 100. Walikuwa ni mchanganyiko wa binadamu na malaika walioasi. Kuzaliwa kwao duniani kulikuwa ni kwa kusudi maalum, lakini kwa bahati mbaya, kusudi hilo halikuwa kusudio la Mungu. Lilikuwa ni kusudi la ibilisi ili kuupinga mpango wa Mungu wa kuleta mbegu itakayo uharibu ufalme wa giza. Hata kama Mungu aliangamiza watu wa kizazi kile akimwacha Nuhu na watoto wake, kwa namna ambayo ibilisi ameendelea kufanya kazi, ameendelea kupenyeza mpango wake hata sasa. Maana yake, anaendelea kuleta watu kinyemela na wakati mwingine kwa njia ya kuzaliwa kama ambavyo wengine huzaliwa. Hao pia wamezaliwa kwa kusudi maalumu, lakini sio kwa ajili ya kusudi la ufalme wa Mungu. Ni kwa ajili ya kusudi la ufalme wa giza. Utakachokiona ni kwamba binadamu yeyote yule hajazaliwa kwa bahati mbaya. Ama amekuja kutekeleza kusudi la ufalme wa giza au kusudi la ufalme wa Mungu. Usipojua umeletwa kwa kusudi gani, unaweza kuiga kusudi lisilokuhusu! Katika kitabu hiki, utajifunza kutambua kusudi la Mungu maishani mwako na namna ya kulitumikia. Soma kwa makini kwa sababu hiki ni kitabu kinachoweza kukusaidia kubali maisha yakeo. Maana wengi wetu tunaishi na kuzalisha chini ya kiwango kinachotakiwa kwa sababu hatujui kusudi la Mungu maishani mwetu. Kwa njia ya kitabu hiki, utapata nafasi ya kuzalisha kile alichokusudia Mungu kwa ajili yako.
| Media | Books Paperback Book (Book with soft cover and glued back) |
| Released | August 11, 2020 |
| ISBN13 | 9798674417033 |
| Pages | 380 |
| Dimensions | 127 × 203 × 22 mm · 412 g |
| Language | Afrikaans |